Kuku ni miongoni mwa ndege wafugwao ambayo wanaweza kuchangia kupunguza ukosekanaji wa ajira kwa Vijana nchini.
- Kuku(tetea) 8 na Jogoo 1
- Banda bora
- Vyombo vya chakula na maji
- Chakula bora
- Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa
- Chanzo cha nishati joto na mwanga
- Elimu na ujuzi wa malezi bora
- Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga
- Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa
- Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu
1 KUKU 8
.. Wakati
wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 8 (matetea) wenye umri sawa na
hawajawai kutaga hatamara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika
familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni
kuzalisha kuku wa kienyeji kwajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa
haraka na yenye uzito mkubwa. Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua
aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi.
1 Ili
kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni
vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao.
Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena watafaa sana maana watakua na umri
mmoja pia.
1 Jogoo
mmoja tu anatosha kuwahudumia kuku matetea yote nane. Hakikisha katika uchaguzi
wa jogoo bora lililochangamka, rangi mzuri, upanga umesimama, macho angavu,
uzito wa kutosha, rangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuzalisha. Ni vema mfugaji
akaelewa kwamba kuku wote watakaozalishwa watategemea ubora wa jogoo wake.
Uwezo wa kutaga kwa kuku na upatikanaji wa mayai pia hutegemea kwa karibu ubora
wa jogoo aliyechaguliwa.
1 BANDA
BORA
2.
Miongoni mwa mambo mhimu naya kwanza
kuzingatiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi ni maandalizi ya
banda bora. Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali.
Mfugaji anatakiwa kuandaa banda lenye ukubwa wa mita 10 kwa mita 04. Yani urefu
uwe mita 10 na upana upana wa mita 04. Kisha kata vyumba vya mita 2 urefu na
upana mita 4 kutoka katika banda lako hivyo utakuwa na jumla ya vyumba vitano
vyenye ukubwa unaolingana. Ujenzi uzingatie malighafi na vifaa vinavyopatikana
kwa urahisi katika mazingira husika
Baadhi
ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-
§
Sakafu: Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito
§
Kuta: Fito, mabanzi, mbao, nguzo
mianzi,udongo, matofali, mawe, mabati na wavu
§
Paa: Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati
na vigae.
§
Wigo: Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi,
mianzi, matete, wavu na mabati
Banda
bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
§
Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na
pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua
pamoja na wanyama hatari.
§
Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha
inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.
§
Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji,
isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.
§
Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika
na kulala.
§
Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji,
kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga.
§
Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi
ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji.
§
Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta
mfupi na sehemu kubwa wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa. Kwenye mazingira
ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi
yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.
No comments:
Post a Comment